MAFUTA YAZIDI KUONGEZA UKALI WA MAISHA NAULI ZA BOTI ZAPAA

 



Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) inatangaza bei mpya za tiketi za boti kwa daraja la chini (Economy Class) zitakazoanza kutumika kuanzia Jumatatu, Mei 11, 2026.


Kwa mujibu wa taarifa ya leo Mei 07, 2026 iliyotolewa na ZMA, bei hizo ni tsh 40,000 kwa abiria wa daraja la kawaida kutoka Tsh 35,000 waliyokuwa wakilipa awali, huku wa daraja la VIP likigharimu Tsh 80,000 kutoka Tsh 70,000 waliyokuwa wakilipa awali.


Vile vile nusu tiketi itauzwa kwa Tsh 20,000, na bei ya Flying Horse imetoka Tsh 20,000 hadi Tsh 22,000. Hata hivyo, watumiaji wa boti kutoka Unguja kwenda Pemba wataendelea kulipa Tsh 40,000 na Pemba kwenda Tanga Tsh 30,000.


Taarifa hiyo imetaja sababu za kupanda kwa bei ya tiketi kuwa ni kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta na kuongezeka kwa bei za uagizaji vipuri kutoka nje ya nchi kuja Tanzania


Aidha bei hizo mpya ni kwa ajili ya boti za abiria ziendazo kwa kasi pamoja na Boti ya Flying Horse tu na hazitahusisha meli za mizigo na abiria ziendazo taratibu (Passenger cargo Ships).


Mamlaka inawaomba wananchi kutoa mashirikiano na iwapo chombo chochote kitakwenda kinyume na bei elekezi zilizoidhinishwa na Mamlaka


Powered by Blogger.