RAIS WA ZAMANI WA BOTSWANA AFARIKI DUNIA.

 

Aliyekuwa Rais wa Botswana, Festus Mogae, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86. Taarifa za kifo chake zimetangazwa na Rais wa Botswana, Duma Boko.


Festus Mogae alihudumu kama Rais wa Botswana kuanzia mwaka 1998 hadi 2008 na alitambulika kwa mchango wake katika kukuza uchumi, utawala bora pamoja na mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI nchini humo.


Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Botswana wameendelea kutoa salamu za pole kufuatia kifo cha kiongozi huyo wa zamani aliyekuwa akiheshimika barani Afrika na duniani kwa ujumla.


Powered by Blogger.