WANNE MBARONI MAUAJI YA M WANAFUNZI WA IFM

 



HABARI: Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa wanne kuhusiana na mauaji ya James Rogers Temba, mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo cha IFM.

Mwili wa marehemu ulikutwa ukielea katika maji ya mto Msimbazi, eneo la Kipawa Ilala Aprili 30, 2026 ukiwa hauna kichwa.


Watuhumiwa waliokamatwa ni Steven Rogers Chaka (31), Anna Frank Lema (30), Twalibu Khamis (23) na Michael John (26), wote wakazi wa Dar es Salaam.


Polisi wamesema uchunguzi unaendelea ili kubaini ukweli wa tukio hilo, na wamewataka wananchi kutoa ushirikiano ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wote watakaobainika kuhusika.

Powered by Blogger.