BEI ZA MAFUTA ZASHUKA DUNIANI



Habari njema kwa watumiaji wa mafuta nchini ambapo kuanzia Jumatano, Julai 1, 2026, bei kikomo za bidhaa za petroli zimeshuka kutokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.


Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), katika kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, imesema kushuka kwa bei hizo kunatokana na mwenendo wa soko la dunia, ambapo petroli imeshuka kwa shilingi 96 kwa lita, dizeli shilingi 151 kwa lita na mafuta ya taa shilingi 242 kwa lita.


EWURA imeeleza kuwa mabadiliko hayo yamechangiwa na makubaliano ya kimataifa kati ya Marekani na Iran kuhusu mgogoro unaoendelea Mashariki ya Kati, pamoja na kuruhusiwa kwa meli za mafuta kupita katika Mlango-bahari wa Hormuz, hali iliyosaidia kupunguza changamoto za usafirishaji wa mafuta duniani.


Hata hivyo, mamlaka hiyo imesema kuwa wastani wa bei za mafuta katika soko la dunia bado haujarejea katika viwango vya kabla ya mgogoro ulioanza Februari 28, 2026. less

Powered by Blogger.