KIJANA MMOJA ATUHUMIWA KUMUUA BABA YAKE KISHA KUMFUKIA CHUMBANI
Na Mwandishi wetu--DAR ES SALAAM:
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limemkamata kijana Juma Ramadhan maarufu @Juli, 21, kwa tuhuma za kumuua baba yake mzee Ramadhan Jafari maarufu @Muna, 47 kwa siri kisha kumfukia chumbani kwake
Akizungumza na Waandishi wa Habari Juni 23,2026 Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro amesema Siri iliyofichika ya kutoweka kwa mzee mmoja eneo la Mbezi Luguruni, Ubungo,Jeshi la Polisi lilifanya uchunguzi wa kina uliodumu kwa takriban wiki moja na kubaini mzee Ramadhan Jafari alifariki dunia katika mazingira ya kusikitisha ndani ya makazi yake eneo la Kwembe.
"Chanzo Kituo chetu Polisi Kimara Gogoni kilipokea taarifa ya kupotea kwa mzee kuanza kufanya uchunguzi mara moja. Wapelelezi kwa kushirikiana na wananchi walifanya ufuatiliaji wa nyumba hadi nyumba, simu hadi simu, hadi ilipobainika kuwa Mzee amefariki na kufukiwa ndani''amesema Kamanda
Kamanda Amesema Katika uchunguzi,Jeshi la Polisi walimkamata kijana Juma Ramadhan maarufu @Juli, ambaye ni mtoto wa marehemu na baada ya mahojiano ya kina, mtuhumiwa alieleza mwenendo wa tukio hilo kwa sasa anashikiliwa huku uchunguzi ukiendelea kubaini sababu kamili zilizosababisha tukio hilo la kusikitisha.
Aidha Kamanda wa Kanda Maalum Jumanne Muliro ametoa shukrani kwa wananchi kwa ushirikiano wao katika kutoa taarifa.
Amesisitiza kuwa hali ya usalama Dar es Salaam kwa ujumla ni nzuri na kwamba mkono wa sheria ni mrefu - mhalifu yeyote atakamata na kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria bila kujali cheo au uhusiano.

