BUNGE LATIMIZA MIAKA 100, ZUNGU ASISITIZA WAJIBU WA KUISIMAMIA SERIKALI

 




Na Mwandishi wetu-Dar es salaam


Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu (Mb), amesema Bunge la Tanzania linaendelea kutekeleza wajibu wake wa msingi wa kuisimamia Serikali na kuhakikisha ustawi wa wananchi, huku akisisitiza kuwa mafanikio ya maendeleo yanayoshuhudiwa nchini ni matokeo ya ushirikiano wa taasisi mbalimbali za dola.




Akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari leo Jumatano katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, kuhusu Maadhimisho ya Miaka 100 ya Chimbuko la Bunge la Tanzania na masuala mbalimbali yanayolihusu Bunge.





Kihistoria Bunge la Tanzania linatimiza miaka 100 mwaka huu tangu kuanza kwake kama Baraza la Kutunga Sheria mwaka 1926 ambapo kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Miaka 100 ya Bunge: Historia Yetu, Dira Yetu".


Aidha, amesema si sahihi kulitaja Bunge kuwa ni dhaifu kwa sababu kila Bunge hutekeleza majukumu yake kulingana na mazingira ya wakati wake, akisisitiza kuwa jukumu kuu la Bunge ni kutunga sheria, kuisimamia Serikali na kuhakikisha ustawi wa jamii.

Powered by Blogger.