KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO MAGOMENI WAWATEMBELEA ASKARI POLISI WATAMBUA MCHANGO WAO
Waumini wa Kanisa la Waadventista wa Sabato kutoka Mtaa wa Magomeni,Julai 29, 2026, wameendelea na ziara yao maalumu ya kuwatembelea na kuzungumza na askari wa Jeshi la Polisi.
Safari hii walifika katika Vikosi vya Polisi Kanda Maalam, Dar es Salaam.
Ziara hiyo imelenga kutambua, kuthamini na kuwapongeza askari wa Polisi kwa mchango wao mkubwa katika kulinda usalama wa raia na mali zao, pamoja na kuimarisha uhusiano kati ya jamii na vyombo vya ulinzi na usalama.
Hatua hiyo imeelezwa kuwa mfano wa mshikamano na ushirikiano unaochangia kujenga jamii yenye amani, upendo na maendeleo.



