MBOLEA YA FOMI YALETA NEEMA KWA WAKULIMA TABORA

 




Na mwandishi wetu, Tabora


WAKULIMA wa zao la tumbaku na mazao mengine Mkoani Tabora wametakiwa kuchangamkia mbolea ya Fomi inayozalishwa hapa nchini na Kampuni ya Itracom Fertilizers Limited kwa kuwa inarutubisha udongo na kupata mavuno mengi zaidi.


Hayo yamebainishwa na Afisa Mauzo wa Kampuni hiyo Mkoani hapa, Yusuph Said, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari walipotembelea Banda la Kampuni hiyo kwenye viwanja vya Maonesho ya Nane Nane Ipuli, Mjini hapa.




Ameeleza kuwa mbolea za Fomi tayari zimeleta mageuzi makubwa kwa wakulima wa tumbaku na mazao mengine katika Mikoa ya Kigoma na Tabora na maeneo mengine walioitumia msimu uliopita kutokana na virutubisho vilivyomo.


‘Mbolea za Fomi ni mkombozi kwa wakulima, kwa kuwa zina mchanganyiko wa mbolea za asili yaani samadi na chokaa, na zimechanganywa na mbolea ya chumvi chumvi hivyo kuwezesha mkulima kupata matokeo chanya na ya haraka,’ameeleza.


Saidi ameongeza kuwa mbolea za Fomi huleta matokeo chanya na ya kudumu shambani hivyo kumwezesha mkulima kupata mavuno mengi, kuvuna majani ya tumbaku yenye ubora wa daraja la juu ambayo yana bei nzuri sokoni.


‘Katika msimu uliopita wakulima waliotumia mbolea hii kwenye kilimo cha tumbaku na mazao mengine walipata manufaa makubwa, hivyo natoa rai kwa wakulima wote kuchangamkia mbolea hizi ili wainuke kiuchumi’, ameongeza.


Amedokeza  kuwa Fomi ni suluhisho la kuongeza tija na mavuno ya mazao ya wakulima, kurejesha rutuba ya shamba, kupata mimea yenye afya na mavuno bora zaidi. Banda la ITRACOM hapa Nane Nane Ipuli lina majibu yote.


Mzee Mohamed Luwanji (78) mkulima wa tumbaku na mahindi kutoka Kata ya Uyowa Wilayani Kaliua Mkoani Tabora amekiri kupata mavuno mengi zaidi ya tumbaku na mahindi baada ya kutumia mbolea hii tofauti na misimu ya nyuma.  



Powered by Blogger.