*MAKAMU MWENYEKITI UVCCM REHEMA SOMBI AWAHIMIZA VIJANA KUWA NA NIDHAMU NA KUSHIRIKI MAENDELEO YA TAIFA*
Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndg. Rehema Sombi Omary (MNEC), amewahimiza vijana kuwa na nidhamu na uzalendo akisisitiza umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika uongozi na maendeleo ya Taifa.
Akizungumza na vijana na mamia ya wananchi Sumbawanga Vijijini wakati wa kufunga kambi ya mafunzo ya vijana, Ndugu Sombi amewapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, kwa kuendelea kuweka kipaumbele katika uwezeshaji wa vijana. Ametolea mfano ongezeko la mgao wa mikopo ya halmashauri kutoka asilimia 10 hadi 15 ya mapato ya ndani, akiwataka vijana kutumia fursa hizo kuimarisha ujasiriamali na kujitegemea kiuchumi.
Aidha, amewataka vijana kukubali kukosolewa na kujikosoa, huku wakidumisha mshikamano na kujiandaa kushiriki kikamilifu katika uongozi na uchaguzi wa mwaka 2027 kwa mujibu wa taratibu husika.
Akizungumzia kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya CCM Sombi amewataka vijana kujitathmini na kujiuliza wamekifanyia nini Chama, wakitazama kilikotoka, kilipo na kinakoelekea.
Ziara hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa Wiki ya UVCCM 2026.
*kaulimbiu “Mazingira Tofauti, Fursa Sawa kwa Vijana.”*
#KaziNaUtuTunasongaMbele



