MZIZIMA FESTIVAL BURUDANI YA KIBABE HAIJAWAHI KUTOKEA DESEMBA 11-13 KUFANYIKA DAR ES SALAAM


 


Na Mwandishi wetu-Dar es salaam


Tamasha la Mzizima Festive linakuja kutoa burudani ambapo ni kwa siku tatu wananchi watuburudila kupitia 

 vikundi 26 vya ngoma za asili, michezo ya jadi, historia ya jiji na mijadala ya maadili kuhusu mmonyoko wa maadili 


Tamasha la Mzizima Festival linalenga, kufuufua, kuenzi na kurithisha mila, desturi na utamaduni wa Watanzania kwa vizazi vya sasa na vijavyo.


Akizungumza leo na Waandishi wa Habari Oktoba 30,2026 Jijini Dar es salaam , Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Pamoja Tutashinda Tanzania (PATUTA) Dr Aida Ndaombwa amesema Tamasha hilo lililoandaliwa na Batuta Organization litajumuisha shughuli mbalimbali za kitamaduni, michezo ya jadi, burudani na mijadala itakayowakutanisha Watanzania wa makabila, rika na umri tofauti, kwa lengo la kuwakumbusha historia ya jamii zao na maisha ya wazee wao.




" tamasha hili litatoa fursa kwa vijana kujifunza michezo ya jadi kama bao, ambayo ilikuwa sehemu ya maisha ya wazee wa wa zamani ikiwemo hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alicheza , na kufahamu historia ya usafiri wa umma jijini Dar es Salaam, ikiwemo chimbuko la daladala, UDA na maendeleo ya usafiri wa mwendokasi"amesema Dr 


Ameongeza kuwa historia ya Dar es Salaam kama kitovu cha biashara pia itajadiliwa, ikiwemo chimbuko na maendeleo ya Soko la Kariakoo pamoja na mchango wa wafanyabiashara kutoka maeneo na makabila mbalimbali.


Aidha, amesema kutakuwa na mijadala itakayowakutanisha wazee na watu waliowahi kushiriki katika shughuli za siasa, utamaduni na majeshi ili kueleza historia waliyoipitia na kuwasaidia vijana kuelewa mabadiliko yaliyotokea katika jamii


Amesema lengo lingine ni kukabiliana na changamoto ya kushuka kwa maadili, akieleza kuwa zamani jamii ziliishi kwa mshikamano kupitia michezo na shughuli za kitamaduni, hivyo ni muhimu kurejesha misingi hiyo kwa kuwashirikisha vijana.


Kwa upande wake, Mratibu wa Tamasha Mayasa Jabiri mratibu amesema Mzizima inawakilisha utamaduni wa ukarimu na historia ya Dar es Salaam, akieleza kuwa wanataka kulitumia jukwaa hilo kuitangaza Tanzania kama nchi yenye amani, fursa za kiuchumi na utamaduni unaowakaribisha wageni.


Amesema jina Mzizima linahusishwa na historia ya eneo hilo na hali ya kutulia au kupoa, akieleza kuwa kupitia tamasha hilo wanataka wageni wanaotembelea Dar es Salaam waondoke wakiwa na kumbukumbu nzuri za ukarimu na amani ya Tanzania.


Pia wanashirikiana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuhakikisha tamasha hilo linafanikiwa na kuonyesha utamaduni halisi wa Tanzania.


Naye Afisa Sanaa BASATA Gabriel Awe amesema baraza hilo limeunga mkono maandalizi ya tamasha hilo baada ya waandaaji kufika ofisini kupata mwongozo kuhusu taratibu za kuandaa na kuendesha matamasha nchini.


Amesema Mzizima Festival ni jukwaa muhimu kwa sababu limegusa masuala ya utamaduni na maadili ambayo kwa sasa ni changamoto katika jamii, hususan kwa kizazi kipya kinachohitaji kufahamu namna wazee wao walivyoishi na misingi waliyokuwa wakifuata.


Ametoa wito kwa wadau na wadhamini mbalimbali kujitokeza kuunga mkono tamasha hilo ili kufanikisha malengo yake ya kuenzi utamaduni na kuunganisha vizazi.


Naye Mdau wa tamasha hilo, Mkurugenzi Mtendaji VOT AFRIKA LIMITED Everest Oende ameyahimiza makampuni na taasisi mbalimbali kutumia Mzizima Festival kama jukwaa la kuonyesha mchango wao katika shughuli za kijamii, akisema ni fursa ya sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika kuhifadhi urithi wa taifa.


Amesema kampuni zinapaswa kujitokeza kuunga mkono Batuta Organization ili tamasha hilo lifanikiwe na kuwa mfano wa ushiriki wa sekta binafsi katika shughuli zinazolenga kuimarisha utamaduni wa Watanzania.


Aidha Watanzania, familia, wadau na wanahabari wanaalikwa kujitokeza kushiriki katika tamasha hilo, akisema anatamani kila familia ipate nafasi ya kushuhudia na kujifunza mambo yatakayowasilishwa.


.

Powered by Blogger.