SENDIGA AWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI MAPEMA ZA EL NINO.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Queen Cuthbert Sendiga amewataka wananchi wa kata ya Lukobe kuchukua tahadhari za mapema kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayopelekea uwepo wa El Nino hapa Nchini.
Mhe. Sendiga amesema hayo katika mkutano na wananchi wa Kata hiyo ikiwa ni ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amesema Serikali kupitia wataalam wa Mkoa huo inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha wananchi wanabaki salama, kwa kuchimba na kupanua mifereji utakayosaidia kutunza maji na kupunguza athari za mafuriko katika maeneo hayo.
Kwa sababu hiyo, amewataka wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi, hususan pembezoni mwa mito, mikondo ya maji na maeneo ya mabondeni, kuchukua tahadhari na kuondoka katika maeneo hayo endapo yatatambuliwa kuwa hatarishi.


