BODI YA NAFAKA YAWAITA WANANCHI MKOANI GEITA KUTEMBELEA BANDA LAO
Na David John timesmajira Online Geita
AFISA masoko na usambazaji kutoka Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko (PCB) Francisco Amos amesema kuwa bodi imejipanga kumuondolea mkulima changamoto ya soko ya mazao yao iliyokuwa inamkabili mkulima huko nyuma
Akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya sita ya teknolojia ya madini yanayofanyika katika viwanja vya EPZA Bobambili mkoani Geita,Amos amesema kuwa Serikali ilianzisha bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko ili iwe jukwaa la wakulima kuuza mazao yao pindi wanapopata changamoto katika masoko au mavuno yao.
"Naweza kusema kwamba tumeshiriki maonyeaho haya tukiwa na lengo la kuonyesha bidhaa bora zinazozalishwa na bodi hiyo kupitia viwanda vyake mbalimbali hapa nchini pamoja na kuwafahamisha fursa mbalimbali ambazo bodi ya nafaka wanazitoa kwa wakazi wa Geita ikiwemo kuuza mazao yao katika bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko huduma za uwakala usambazaji na vilevile tunatoa ushauri wa kitalaamu wa maswala ya kilimo na mambo mengine kama hayo "Amesema Amos
Nakuongeza kuwa "Tunawaomba wakulima mkoani Geita na wale wote wanaofika katika maonyesho kutembelea banda letu ili kufahamu fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya kilimo hususani katika suala zima lakuongeza thamani ya mazao ambapo kimsingi ndio jukumu mama la bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko."Amesisitiza Amos.
Pia ameongeza kuwa wao pamoja na wadau wengine wa sekta binafsi wananunua mazao katika bei shindani ambapo amewasisitiza wakulima kuendelea kulima kutokana na soko la mazao lipo na wao kama CPB wapo tayari kununua.
Ametoa msisitizo kwa wakazi wa Kanda ya ziwa kuendelea kulima zao la mpunga wakutosha nakwamba Bodi ya nafaka ipo tayari kununua kwa bei shindani hivyo muhimu kutembelea banda hilo kujua namna gani mazao yao yanaweza kupata vigezo vya kununuliwa na bodi hiyo kutokana na kuwa na viwango vyao vya ubora.
Hata hivyo amewataka wakulima nchini kuwa na utaratibu wakukutana na wataalamu wa ubora ambapo watawapa ushauri kwa ni namna gani walime kuanzia shambani kuvuna ili mazao yao yanapoingia sokoni yawe na ubora unaotakiwa yaweze kuwa shindani katika soko.