WANANCHI GEITA ,WAFURAHIA HUDUMA YA RITA

 


Na David John Geita

WAKALA wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) umewataka wananchi Kujenga desturi ya kuandika wosia Ili kuondoa migogoro ya mirathi inayochukua muda mwingi kufuatilia kesi mahakamani na  badala ya muda huo kuutumia kwenye shughuli za uzalishaji Mali.

Hayo yamesemwa na Wakili wa Serikali kutoka RITA  Salvius Rwechungura wakati akizungumza na waandishi wa Habari kwenye maonyesho ya sita ya Kimataifa na Teknolojia ya madini  yanayoendelea mkoani Geita.

 "Sisi kama Rita tuna kaulimbiu yetu  inasema 'kuandika wosia siyo uchuro'ikiwa na maana kwamba kuandika wosia ni utaratibu  ambao binadamu anatakiwa awe nao ili kujua siku asipokuwepo mali zake zinagawanywa katika utaratibu bila kuleta migogoro."amesema Rwechengura

Nakuongeza kuwa "Tunashuhudia katika vyombo vya habari watu wanagombania Mali alizoacha marejemu lakini kumbe angekuwa ameacha waraka kwamba Mali zinagawanywaje migogoro kwenye jamii isingekuwepo na watu wasingetumia muda miwngi kugombana  kwa kwenda mahakamani kudai mali ambazo zingegawanywa kwa utaratibu unaoeleweka"Amesema 

Pia   Rwechengura amesema pamoja na kutoa huduma na ushairi katika kuandika wosia pia RITA inajihusisha na usajili wa matukio mbalimbali ya binadamu ikiwemo kuzaliwa,kufa ,ndoa na talaka , huduma za kuasili watoto na vile vile RITA inatoa huduma ya ushauri katika suala la ufilisi na masuala ya bodi za wadhamini.

"Kwa hiyo kwa kifupi sisi kama RITA tunahudumia watu wengi ambao wanakuja hapa wanahitaji kusajili vyeti vya kuzaliwa ambavyo vinasaidia katika mchakato mzima wa kupata huduma nyingine kama kitambulisho Cha utaifa ( NIDA) , namba za utambulisho wa mlipa Kodi na masuala mengine ambayo yanasaidia kupata hati za kusafiria,

"Kwa hiyo ukiangalia kwa upana wake hizo huduma zinawahusu pia wachimbaji na wafanyabiashara kwa sababu wakiwa wamesajiliwa maana yake wametambuliwa, basi Serikali inapata nafasi ya kuwatambua watu inayowahudumia katika sekta mbalimbali zikiwemo sekta za madini."Amesema 

Nakuongeza kuwa "Niseme tu RITA imehamia Geita vyeti vya kuzaliwa vinatolewa kama mnavyoona ndani ya muda mfupi kikubwa aweze kufika na viambatanisho stahiki vinavyowezesha kupata huduma ya cheti Cha kuzaliwa ." Amesisitiza Rwechengura 


Naye Mwananchi aliyekuwa katika Banda hilo akipata huduma Lilian Ndila  ameishukuru Serikali kwa kuleta maonyesho hayo kwani yanasaidia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata vyeti vya kuzaliwa kwa urahisi.


"Mimi nashukuru leo nimepata cheti cha kuzaliwa cha mwanangu  kwa siku mbili tu ,wakati nimeshafuatilia kwa takribani miezi miwili bila mafanikio."amesema Ndila  



Powered by Blogger.