28 WAVISHWA NISHANI POLISI

 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura Mei 27, 2024 amewavalisha nishani Maofisa, wakaguzi na askari 28 wa vyeo mbalimbali  kwa niaba ya Mhe. Rais na Amiri Jeshi Mkuu.

Nishani hizo zilitolewa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.





Aidha, hafla ya uvishaji wa nishani hizo ilifanyika mkoani Mbeya ambapo ilihusisha Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yenye mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya na Njombe.

Powered by Blogger.