"NJOONI MTOE USHAHIDI- WANANCHI WAASWA


Na Mwandishi Wetu Zanzibar. 

Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar DCP Zuberi Chembera amekutana na kuzungumza na Wakuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mikoa, Wilaya na Vituo katika kikao kazi kilichofanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar

Mei 28, 2024 ambapo amewakumbusha kuhusu wajibu wao hasa katika eneo la upelelezi wa makosa ya kijinai.


Naibu Kamishna Chembera amesema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya mashahidi wa kesi mbalimbali kutofika kutoa ushahidi Mahakamani hali inasababisha kesi kushindwa kuendelea mahakamani na watuhumiwa wa makosa mbalimbali kuachiwa huru .
Naye Mkurugenzi wa makosa wa makosa ya jinai mkoa wa Kaskazini Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Omari Khamis Abdalah kuacha muhali na kuzimaliza kesi kwa mapatano na badala yake wafike mahakamani kutoa ushahidi ili watuhumiwa wapate kuhukumiwa na makosa wanayotuhumiwa nayo

Powered by Blogger.