POLISI WAONGEZA MUDA WA KUOMBA AJIRA



 Jeshi la Polisi Tanzania limetoa tangazo la kuongezwa kwa muda kuomba ajira katika jeshi hilo kutoka tarehe ya mwisho Mei 21 hadi 26 mwaka huu.

Awali, Mei 15 Mkuu wa Jeshi hilo alitoa tangazo la nyongeza ya siku tano (5), lakini kutoka na shida ya mtandao zikaongezwa hadi Mei 26.

"Kutokana na changamoto ya mtandao inayoendelea kujitokeza, mnatangaziwa kuwa vijana wenye sifa na nia ya kujiunga na jeshi la Polisi, zimeongezwa siku tano za kuendelea kutuma maombi," inaeleza sehemu ya tangazo hilo la Mei 21, 2024 kutoka Makao Makuu ya Jeshi hilo Dodoma
 

Powered by Blogger.