BAJETI YA YANGA 2024/25 'KUFURU'
Na Mwandishi Wetu Dar
Klabu ya Yanga leo Juni 9, 2024 imefanya Mkutano Mkuu ambapo Rais wa mabingwa hao mara 30 wa Ligi Kuu Tanzania Bara Inj. Hersi Said ameelezea mwelekeo wa klabu yao kuelekea msimu wa 2024/25.
"Klabu yetu inahitajika kujengeka kiuchumi. Kazi yetu kama viongozi ni kuhakikisha tunapata wadhamini ambao watasaidia na mfadhili wetu GSM. Lakini mashabiki wetu pia wanao mchango mkubwa kwa kuhakikisha kuwa kupitia ada za Wanachama tunapata mapato ya kuendesha klabu yetu" Injinia Hersi Said
Pamoja na mambo mengine, wajumbe wa mkutano wameelezwa mapato na matumizi kwa msimu wa uliopita
Ufuatao ni mchanganuo kwa ufupi mapato ya Yanga kwa msimu uliopita na bajeti ya msimu ujao;
"Udhamini na haki za matangazo bilioni 10.19, Mapato mlangoni bilioni 1, Ada za Wanachama milioni 613, Zawadi za ushindi bilioni 3.9
Mapato mengine bilioni 5
Jumla ya mapato ni Bilioni 21
MATUMIZI:
Pesa ni katika bilioni za shilingi
7.39 Mishahara, 3.5 Usajili na uhamisho wa wachezaji
2.89 Usafiri, Chakula na Malazi
1.85 Maandalizi ya mechi 2.6, Motisha 0.702, gharama za kambi 0.944 .
Matumizi mengine ni, Compliance 1.46 Bil. kiutawala
0.424, masoko na 0.503 kifedha
Jumla ya matumizi ni shilingi 22.28 bilioni.
Kwa hiyo, Mapato ukiondoa matumizi inaonekana Klabu imepata hasara ya 1.28 bilioni
Wakati huo huo, imetangazwa kubwa bajeti ya Msimu ujao ni Bilioni 24.5 ambapo imeongezeka asilimia kumi tofauti na Msimu uliopita ambayo ni Bilioni 22.