SIMBA KWAZIDI KUFUKUTA

 Anaandika Dr.Hamis Kigwangalah katika ukurasa wake wa X (Twitter).

"Kama ni kudaiana tu, tena bila mikataba, basi na sisi wana


SimbaSC tunamdai mwekezaji pesa nyingi sana!

Tulimtaka aweke bilioni 20 kwenye account yetu ili tununue bonds, kumbe hakuweka! Kama angeweka tungenunua bonds za miaka 25, at a coupon rate of 15.95% tungepata faida ya bilioni 3.19 kila mwaka. Kwa miaka 7 aliyotuzubaisha bila mafanikio yoyote yale, tungevuna bilioni 22.33!

Deni la pili; ni pesa alizotukosesha kutokana na ufadhili wa Azam - bilioni ngapi? Kwa mwaka ni bilioni 3. Kwa miaka 7 ni bilioni 21!

Na yeye matangazo yake alikuwa analipia ufadhili kiasi gani?

Tayari kwa haya mawili tu, tunamdai mwekezaji Glezabhai zaidi ya bilioni 43.33! Taja na wewe madeni mengine tunayomdai Glezabhai ili twende sawa!

Halafu, Wajumbe wa Bodi waliokurupuka leo kutoka usingizini tuna jambo nao: watuambie walimpa Glezabhai mamlaka ya kumiliki timu yetu kwa msingi upi? Maana hakufuata prospectus ya mchakato wa transformation wa kampuni inavyotaka.

Nimemuona Ndugu Issa akitumia Memorandum ya kampuni…how? Kama mchakato wa kulipia hisa haujakamilika hiyo document haina nguvu yoyote ile, ile bodi yao waliyokuwa wanakaa haina maana yoyote ile. Na wala Simba Sports Club haijauzwa na wala haidaiwi na mtu - kimsingi tumerudi GROUND ZERO!

Ile bodi ilikuwa genge la watu walioiteka tu timu yetu kinyemela. Kwa taarifa za Ndg. Issa, maana yake Glezabhai hana haki wala mamlaka yoyote yale kisheria kwenye Simba. Simba SC ni club ya wanachama kwa asilimia 100.

Wanachama tunamtaka Ndg. Mangungu aitishe mkutano mkuu haraka tuamue hatma ya club yetu. Kwenye mkutano huo aandae hesabu za mapato na matumizi ya Simba….kuanzia viingilio vya getini siku za mechi, mikataba ya mauzo ya bidhaa, mikataba ya mauzo ya haki za matangazo (ikiwemo ya bidhaa za Glezabhai, mbet nk), mapato ya CAF (robo fainali zote), n.k.

Ndg. Mangungu na Kamati Tendaji wakishindwa kufanya hivi, tutaingilia kati kwa kuunda ‘kikosi kazi’ maalum (task force) cha kuiokoa club yetu".

Glezabhai ni nani?

Tunafuatilia  

Powered by Blogger.