EWURA YAENDELEA KUHAMASISHA MATUMIZI YA GESI KATIKA MAGARI
Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imesema kuwa katika wanaendelea kuhamasisha watu wenye magari nchini kurekebisha mifumo ya magari yao ili kuweza kutumia gesi asilia.
Haya yamesemwa jijini Dar es Salaam leo Julai 5, 2024 na Meneja Mawasiliano na Uhusiano EWURA Titus Kaguo katika maonesho ya 48 ya kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF), kwenye banda la mamlaka hiyo.
Amesema Shirika la Viwango Tanzania (TBS), tayari lilishaboresha viwango vya ubora ambapo kituo chochote cha mafuta nchini kinaweza kujumuisha kituo cha gesi asilia katika eneo moja (CNG).
Kaguo amesema pia kuwa ili CNG iweze kutumika nchi nzimaitaekwenda kwa awamu , na kwa mujibu wa maelekezo ya wizara, EWURA isimamie suala hili kama chanzo kingine mbadala cha nishati safi kutokana na hali mafuta duniani.
Aidha ameiwashukuru Watendaji wa Wizara ya Nishati kwa utendaji bora na , kwa miongozo ambayo wizara imeendelea kuipatia EWURA ili kuendelea kufanya kazi ya udhibiti wa huduma nishati na maji vizuri.
Kaguo amesema kuwa katika banda hilo wataalam wote wapo wa gesi asilia, sekta ya maji, petroli, huku akisema wamejipanga kutoa elimu na kuhakikisha kila changamoto inatatuliwa.
" Tumekuja hapa kwa maelekezo maalum kama tunavyojua Wizara ya Nishati imejipanga kutoa taarifa kwa Umma, taarifa hizi ni nyenzo kwa shughuli ambazo tunazifanya kama tunavyoagizwa na kiongozi wetu, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mh.Doto Biteko,"amesema
Ameeleza kuwa hata alivyokuwa akizindua ripoti za taarifa za utendaji wa nishati moja ya maelekezo yake ilikuwa kuzitaka taasisi zitoe taarifa kwa umma ili watanzania wajue wizara inachokifanya.
EWURA imeshiriki katika maonesho haya,ikiwa ni moja ya nyenzo ya kuwasiliana na kupokea mrejesho kutoka kwa wadau wake kuhusu udhibiti wa huduma za umeme,petroli,Gesi Asilia na Maji na Usafi wa Mazingira.