MAITI 8 ZILIZOFUNGWA KWENYE VIROBA KENYA NI ZA WANAWAKE
BBC:
Kaimu Mkuu wa Polisi, Douglas Kanja ametoa matokeo ya uchunguzi wa awali ambao unaonesha kuwa maiti zote nane zilizopatikana katika jalala la Kware jijini Nairobi zilikuwa za kike ambazo zilikatwa vipande vipande.
''Nimewahamisha maafisa kutoka Kituo cha Polisi cha Kware ili kuhakikisha uchunguzi wa haki na usawa'' alisema mkuu huyo
Itachukua siku 21 kwa polisi na mashirika ya uchunguzi nchini Kenya kutegua kitendawili cha miili hiyo.
Katika hotuba kwa vyombo vya habari Jumapili, Kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja na Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) Mohamed Amin walihakikishia umma kwamba uchunguzi kuhusu mauaji hayo unaendelea, na baadhi ya watu wanaohusika wametambuliwa.
Tukio hilo limeweka shinikizo kwa Rais William Ruto, ambaye ameapa kwamba wale waliohusika na mauaji hayo wataadhibiwa.
"Sisi ni nchi ya kidemokrasia inayoongozwa na utawala wa sheria. Wale waliohusika katika mauaji ya kutatanisha Nairobi na sehemu nyingine yoyote ya nchi watawajibishwa," alisema katika chapisho kwenye ukurasa wa X, zamani Twitter.
Kisa hicho ni tukio la hivi karibuni la kuhuzunisha nchini Kenya.
Mwaka jana nchi iliachwa na hofu baada ya mabaki ya mamia ya watu wanaohusishwa na ibada ya siku ya maangamizi kugunduliwa katika mji wa pwani wa Bahari ya Hindi wa Malindi. Paul Nthenge Mackenzie alifikishwa mahakamani mjini Mombasa mapema wiki hii kwa tuhuma za ugaidi na mauaji kutokana na vifo vya wafuasi wake zaidi ya 440.
Anakanusha madai hayo. Anadaiwa kuwahimiza wanaume, wanawake na watoto kujinyima kula ili "kukutana na Yesu", katika moja ya vibaya zaidi duniani vinavyohusiana na ibada.