CHADEMA YAZUIWA NGORONGORO
POLISI NGORONGORO WAZUIA MKUTANO WA HADHARA WA CHADEMA
Chama cha Demokrasia na Maendelea (Chadema) kupitia kwa Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema kilitarajia kufanya mkutano wa hadhara katika Kata za Ngorongoro eneo la Oloirobi na Kata ya Alailelai eneo la madukani Agosti 30, 2024.
Barua ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ngorongoro, SSP L.N. Ncheyeki kwenda Chadema Kanda ya Kaskazini ilisema, jeshi hilo limesitisha mikutano ya hadhara kutokana na kuwepo shughuli za kuimarisha usalama Wilayani humo.
Hata hivyo, Lema amsema atalizungumzia suala hilo leo katika mkutano wa wanahabari.