KAMPENI YA WEWE NI WA THAMANI KUBADILISHA TABIA ZA VIJANA NCHINI

 


Na Mwandishi wetu,DAR ES SALAAM 

MKURUGENZI  wa Kampeni ya 'Wewe ni wa Thamani'  Aziza Suedi amesema wanatarajia kuzindua kampeni hiyo hivi karibuni kwa lengo la kurudisha imani kwenye miyoyo ya  vijana kutokana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo na kuwasababisha waweze kukataa tamaa.

Akizungumza na Mwandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,amesema Kampeni hiyo inaendeshwa na vijana wa Kitanzania  ambao wameshuhudia   vijana wengi wakiwa wanaingia katika makundi mabaya mbali mbali ambapo inapelekea kujihusisha na madawa ya kulevya, Utumiaji wa pombe kali na kujiunga makundi mengine yasio na faida kwao wala kwa jamii.

Amesema kampeni hiyo imejikita  katika kumsaidia kijana wa kitanzania kuijuia thamani yake  na kujua mchango wake kwenye jamii na taifa kwa ujumla. 

"Natoa wito kwa wadau wa  maendeleo wote nchini kuungana nao katika harakati za kumtengenezea kijana mazingira mazuri ili awe faida kwao na jamii inayowazunguka ,"amesema.

Aidha amesema kampeni hiyo ni ya nchi nzima hivyo itakuwa ya awamu kwa awamu ambapo itaweza kuwafikia vijana wengi zaidi.

"Kampeni hii tunatarajia kuzindua  mwezi ujao ambapo tunaamini vijana watabadilika na kuchukua hatua  stahiki za kuwasaidia kutimiza ndoto zao,"amesema.

Powered by Blogger.