POLEPOLE AMTEMBELEA MJANE WA CHE GUEVARA


HAVANA: Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Mhe. Humphrey Polepole amemtembelea na kufanya mazungumzo na Mjane wa Mwana Mapinduzi Ernesto Guevara de la Serna au “Che Guevara”, Mama Aleida March (katikati) pamoja na Binti yake Aleida Guevara March.

Katika mazungumzo yao, Mama Guevara amesema anaikumbuka sana Tanzania na kuwa alikuwa na wakati mzuri sana Tanzania alipokuja kumsalimu Che nchini Tanzania. 

Aidha, Mama Aleida March amethibitisha kuhudhuria Kongamano la Kimataifa la Kiswahili - Havana litakalofanyika baadaye Mwezi Novemba 2024. 

Powered by Blogger.