KUPOTEA WATU: TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA KUCHUNGUZA
Dodoma. Jaji Mathew Mwaimu ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora amesema kuwa wanaendelea na uchunguzi wa matukio ya kupotea kwa watu yanayoripotiwa nchini.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma, amesema kuwa lengo la kufanya uchunguzi huo ni kubaini chanzo na wahusika wa matukio hayo ili kutoa mapendekezo stahiki kwa mamlaka husika.
Jaji Mwaimu amesema, chunguzi ambazo zinaendelea kwa sasa zinahusisha mikoa ya Dar es salaam, Singida, Mara, Shinyanga, Mwanza, Kagera, Geita, Kigoma, Tanga, Mbeya, Iringa, Kilimanjaro, Arusha, Ruvuma na Rukwa.