BOT YATOA MAFUNZO YA UTAMBUZI WA ALAMA KWENYE NOTI KWA WATU WA CHANGAMOTO YA ULEMAVU

 


Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeendesha mafunzo maalum kwa wanachama wa Chama cha Wanawake Wenye Changamoto ya Ulemavu (VIDIWOTA) jijini Mbeya, yaliyolenga kuwasaidia kutambua alama za usalama kwenye noti na sarafu, kupata mikopo kutoka taasisi zinazosimamiwa na Benki Kuu, na kuelimishwa kuhusu uwekezaji katika dhamana za serikali.

Kaimu Mkurugenzi wa Tawi la Benki Kuu Mbeya, Dkt. Nicholaus Kessy, alifungua mafunzo hayo  yaliyofanyika katika Tawi la BoT Mbeya na kuhudhuriwa na wanachama 70 wa VIDIWOTA.


Dkt. Kessy alisisitiza kuwa mafunzo hayo ni muhimu katika biashara zao, kwani yatawakinga dhidi ya udanganyifu wa kupokea fedha bandia.

Powered by Blogger.