NGORONGORO HATIMAYE WAREJESHEWA HAKI YA KUSHIRIKI UCHAGUZI

 ARUSHA: Wakazi wa Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha wamerejeshewa Haki yao ya kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na nyingine zijazo baada ya Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mh. Mohamed Mchengerwa kutangaza hatua hiyo leo Septemba 16, 2024.

Mchengerwa ametangaza kurejesha Tarafa 3, Kata 28, Vijiji 65 na vitongoji 242, ambapo wananchi wa maeneo hayo watashiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Awali Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa kupitia tangazo  lililochapishwa kwenye Gazeti la Serikali namba 673 la tarehe 2 Agosti 2024, alitangaza kufuta Vijiji vyote na vitongoji vya Wilaya hiyo inayokaliwa kwa asilimia kubwa na watanzania jamii ya Wamasaai wanaojishughulisha zaidi na ufugaji.



Powered by Blogger.