'KUNYWA' MAFUTA MTINDO WA KIDEBE MARUFUKU

 


Na Mwandishi Wetu
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(EWURA) imepiga marufuku vituo vyote vya mafuta kujaza nishati hiyo kwenye vyombo visivyoruhusiwa kisheria ili kuepusha madhara yanayoweza kusababishwa na hatua hiyo.
Katika taarifa yake kwa umma, EWURA imetaja baadhi ya vifaa visivyofaa kujazia nishati yaafuta vituoni kuwa ni pamoja naadumu na chupa za plastiki.

"EWURA inawakumbusha wamiliki wote wa vituo vya mafuta kuzingatia matakwa ya Kanuni Namba 27 kwa kutoruhusu uuzwaji wa mafuta ya petroli kwenye vifaa visivyoruhusiwa kuchukulia/kuhifadhia mafuta kama vile madumu, chupa za aina zote na vifaa vingine visivyoruhusiwa kisheria."
Soma👇 Taarifa nzima ya EWURA




Powered by Blogger.