MGANI: KIPINDI CHA UCHAGUZI NDOA ZA UTOTONI,UKEKETAJI TARIME UONGEZEKA
NA MWANDISHI WETU,Mara
IMEELEZWA kuwa wanasiasa wanaonekana kuwa chanzo kikubwa cha uwepo wa ndoa za utotoni na ukeketaji katika wilaya ya Tarime kwa kushindwa kuyaongea kwa jamii kwa lengo la kulinda nafasi zao.
Ambapo, kwa miaka ya uchaguzi mara nyingi kumekuwa na ongezeko la wahanga wengi wanaopitia masuala ya ukeketaji na ndoa za utotoni kutokana na wanasiasa kuyafumbia macho masuala hayo kwa kulinda kura zao.
Akizungumza jana wilayani Tarime, Meneja wa Miradi Shirika linalopinga Ukeketaji la Terminationof Female Genital Mutilation(ATFGM) Wilayani Tarime Mkoani Mara,Valerian Mgani wakati wa Mtandao wa Kutokomeza Ndoa za Utotoni Tanzania (TECMN) walipofanya ziara katika Kituo chao kinachopokea wahanga wa ukeketaji na ndoa za utotoni kutoka maeneo mbalimbali ambapo wasichana hao ukimbilia mahali hapo kama sehemu ya kujiokoa na matukio hayo kutopata.
Mgani amesema wanasiasa kuyafumbia macho mambo hayo yanakuwa sababu yankuongezeka kwa kiasi kikubwa kwa wilaya hiyo.
"Kila mwaka wa uchaguzi kumekuwa na changamoto hii kuwa kubwa ,Mfano mwaka 2020 kumekuwa na changamoto kubwa ya idadi ya watoto kukimbilia katika kituo hicho kutokana na wengi kutaka kukeketwa na wengine kuozeshwa wakiwa na umri mdogo na hii inatokana na watu kuwa bize na masuala ya siasa na kushindwa kuwatetea watoto,"amesema.
Amesema kwa mwaka huu hali hiyo imeanza kuonekana mapema hivyo wao kama asasi na kituo wanategemea kupokea wahanga wa masuala ya ukeketaji na ndoa za utotoni zaidi ya watoto700 kituoni hapo.
Kwa upande wake Mratibu wa Mtandao huo,Lilian Kimati amesema lengo la Caravan hiyo ni kupita katika mikoa minne ambayo ina asilimia kubwa ya ndoa za utotoni ikiwemo mkoa wa Mara ,Shinyanga,Tabora na Dodoma.
"Mtandao wao ulianzishwa mwaka 2012 na kipindi hicho kulikuwa na changamoto kubwa ya ndoa za utotoni hivyo walijiunga kwa lengo la kuwa na sauti moja ili kutokomeza ndoa hizo za utotoni ambapo ulianzishwa na mashirika 12 ila kwa sasa mtandao unamashirika 87 ambayo unafanya kazi Tanzania nzima na Zanzibar,"amesema
Amesema miongoni mwa mashirika ambayo yameongoza katika Caravan hiyo ni pamoja na wanachama wa Mtandao huo kutoka Shirika la Msichana Initiative,Binti Makini,Medea,Plan Internationa, My Legacy na Theatre Arts Feminist Group