ARENA YA KISASA KUJENGWA TANGANYIKA PAKERS



Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa taarifa kuwa Ukumbi (Arena) wa burudani wa kisasa uko mbioni kujengwa katika viwanja vya kilichokuwa kiwanda cha kuchakata nyama cha Tanganyika Pakers vilivyoko Kawe Jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza jana katika viwanja vya Leaders Club kwenye onyesho la vicheksho la Cheka Tu, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma alisema Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa idhini kwa Wizara hiyo kuanza mchakato wa ujenzi wa jumba hilo kubwa la burudani.

Waziri Mwinjuma alisema, Mhe Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ni mpenzi na kiongozi anayejali vijana wanaojishughulisha na kazi za sanaa na michazo kwa ujumla, ameagiza ujenzi wa Arena hiyo uanze mara moja.


Katika hatua nyingine, Rais mstaafu wa JMT awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amempongeza Rais Dkt. Samia kuja na wazo la kujenga Arena kwa sababu itakuwa ndiyo suluhisho la kilio cha muda mrefu cha wasanii ambao wanahitaji sehemu kubwa ya kuonesha vipaji vyao.

"Na mimi kwa kuwa naishi karibu na Tanganyika Pakers, nitakuwa nakuja Kawe Arena kwa miguu," alisema Mhe Kikwete.

Kipindi cha Cheka Tu kinaonyeshwa kwenye chaneli ya Cheka Plus namba 414  katika kisimbuzi cha Azam


Powered by Blogger.