BREAKING: KINDIKI ATEULIWA NAIBU RAIS KENYA; MAHAKAMA YAPIGA 'STOP'

 


KENYA: Wabunge nchini Kenya muda mfupi uliopita wamepiga kura kwa kauli moja kuafiki uteuzi wa Profesa Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais mpya.

Wabunge wote 236 waliokuwa bungeni wamepiga kura kuunga mkono uteuzi wa Rais

Hii ni baada ya Rais William Ruto kuwasilisha jina la Profesa Kindiki kwa Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangula kupendekeza achukuwe wadhifa huo.

Nafasi ya Naibu Rais iliachwa wazi baada ya Rigathi Gachagua kuondolewa madarakani kupitia mchakato wa kikatiba.

Kilichosalia sasa ni Spika wa Bunge kuchapisha hatua hiyo katika Gazeti rasmi la serikali.

MAHAKAMA YAPIGA 'STOP'


  1. Mahakama kuu imesitisha utekelezwaji wa azimio la Seneti la kuidhinisha mashtaka ya kumuondoa madarakani Rigathi Gachagua.

    Uamuzi huo umetolewa muda mfupi tu baada ya Bunge la Kitaifa kuafiki uteuzi wa Kithure Kindiki kuwa Naibu wa Rais baada ya Rais William Ruto kuwasilisha jina lake kwenye bunge hilo.

    Hapo jana Maseneta nchini humo waliidhinisha mashtaka 5 kati ya 11 dhidi ya Gachagua na kumuondoa ofisini.

    Gachagua alikosa kufika mbele ya maseneta kujitetea baada ya mawakili wake kusema alipatwa na ''maumivu makali ya kifua'' na kulazimika kulazwa hospitalini.

    Uamuzi uliotolewa na Jaji E.C. Mwita umezuia kutekelezwa kwa azimio hilo la seneti na pia kuzuia rais kumteua mtu kuichukua nafasi hiyo hadi tarehe 24 mwezi huu hadi kesi hiyo sikilizwe na jopo la majaji watakaoteuliwa na Jaji Mkuu Martha Koome.

    Hata hivyo tayari rais amependekeza jina la Kithure Kindiki kuichukua nafasi ya Gachagua na bunge la taifa kuafiki uteuzi wake.



Powered by Blogger.