WANANCHI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI ZA KUJIKINGA NA UGONJWA WA MARBURG,MPOX

 

Na Mwandishi wetu,DAR ES SALAAM 

WANANCHI wametakiwa kuchukua tahadhari pamoja na kujikinga dhidi ya tishio la mlipuko wa magonjwa ya Marburg na Mpox.

Wito huo umetolewa Jijini Dar es salaam na  Kaimu Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya elimu ya afya kwa umma_ Idala ya Kinga Wizara ya afya Dkt Ona Machangu wakati akifungua semina ya wanahabari na wahariri kuhusu taadhari dhidi ya tishio la mlipuko wa ugonjwa wa Marburg na Mpox.

"Naiomba jamii kuwa na utaratibu wa kufika katika vituo vya afya na kutoa taarifa kwa watoa huduma za afya pindi mnapoona  dalili za magonjwa hayo kama kutokwa na vipele mwilini, kuchoka mwili, kutoka na damu puani au masikioni pamoja na dalili nyingize za magonjwa hayo ili watoa huduma wa afya waweze kumpatia matibabu"alisisitiza  Dkt Machangu

Pia amesema Wizara ya afya imekuwa ikiendelea  kutoa elimu katika jamii na kuhamasisha jinsi ya kujikinga na magonjwa ya kuambukiza .


"Tanzania ni moja ya nchi katika ukanda wa Afrika mashariki ambao umezugukwa na nchi mbalimbali ambazo zimekuwa zikikubwa na matishio ya ugonjwa wa Marburg na Mpox"amesema Machangu 

Vilevile amesema Nchi ya Tanzania kwa sasa ipo salama na kusisitiza  kuwa timu ya wataalamu wa afya imeendelea kujiimarisha katika mikoa mbalimbali ambayo inapakana na nchi ya Rwanda kutokana na kukubwa na ugonjwa wa Marburg na Mpox.

Dkt Machangu amewaomba wahariri  na waandishi wa habari kutumia taaluma zao kuweza kuifikishia jamii elimu na hamasa juu ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko hususan Mpox na Marbug.


Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Afya Englibert Kayombo amesema kuwa semina hiyo ya waandishi wa habari ni endelevu na taratibu za Wizara kukaa pamoja na wadau hao ili kuwapa elimu muhimu itayawasaidia katika kutoa taarifa kwa usahihi.

Naye James Mhilu, Mratibu wa Mafunzo hayo amewataka Waandishi wa habari na Wahariri kuwakumbusha wananchi kupiga namba 199 kituo cha miito ya simu cha Wizara ya Afya (Afya Call Center) kwa taarifa, maoni na ushauri zaidi. 

Powered by Blogger.