WASIRA AKIPONGEZA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE KWA KUENZI FALSAFA ZA BABA WA TAIFA

 


Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM 

Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA). Stephen Wasira amekipongeza Chuo hicho kwa kuendelea kuenzi na kusimamia Maono na Falsafa za baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage  Nyerere katika kuhakiksha chuo hicho kinaendeleza na kusimamia masuala ya Uongozi, Maadili na Utawala.

Mzee Wasira ameyasema hayo kwenye kongamano la tatu la Kitaaluma la kumbukizi ya baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere  ambalo liliambatana na uzinduzi wa Kitabu kinachoelezea falsafa ya Mwalimu Nyerere katika kuboresha Maisha ya Watu, Maendeleo ya Kiuchumi, Kisiasa na Kijamii.

Amesema Wakati Taifa likiendelea kumuenzi Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baba wa Taifa JK Nyerere, Tanzania imeendelea kutekeleza kwa vitendo na kuendeleza falsafa zilizoachwa na Hayati Nyerere kwa kuhakikisha Taifa linaishi kwa Maridhiano, Mabadiliko,  Ustahmilivu, na Kujenga upya (4R) ambazo Rais Samia amekuwa akizisimamia.

" Ni wazi kuwa pamoja na kutokuwa pamoja na baba wa Taifa kwa miaka 25, mambo mengi aliyotuachia ikiwemo Misingi ya Uongozi na  kuhakikisha  Umoja  unaeendelezwa  kwa vitendo ikiwa ni pamoja na 4R ambazo zimekuwa zikisimamiwa na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, alisema Mzee Wasira.


Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho Prof. Shadrack Mwakalila amesema mada kuu katika Kongamano hilo ni 'Maono ya Mwalimu Nyerere katika Uongozi na Maendeleo Endelevu' na kuwa Chuo kimeendelea kujivunia misingi mizuri aliyoiacha Baba wa Taifa  ukiwepo Umoja,Upendo na Mshikamano.

 Prof. Mwakalila ameeleza kuwa chuo kimeandaa kongamano hilo kwa lengo la Kumuenzi baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

Amesema Chuo kimeendelea Kuenzi misingi ya Uongozi na Utawala bora, maono ya Mwalimu Nyerere kuhusu kujitegemea. utunzaji wa mazingira kwa ustawi wa jamii na  Maendeleo ya kiuchumi. 

Aidha ni jambo la kumshukuru Mungu kuwa uongozi wa Taifa la Tanzania umeendelea kuenzi misingi ya Baba wa Taifa kwa kudumisha amani, umoja, upendo na mshikamano katika ujenzi wa Taifa.


Naye Mratibu wa Kituo Cha Ukombozi Barani Afrika, Christopher Mhongole amesema Makongamano ya aina hii yana umuhimu mkubwa sana kwa vijana, kwa kuwa vijana walio wengi hawamfahamu vizuri Baba wa Taifa, badala yake wanamsoma na kusikiliza baadhi ya hotuba zake, hivyo kupitia makongamana ya namna hii yanayofanywa na Chuo yanawasaidia na kuwajenga vijana katika misingi na Maadili yanayotakiwa katika Taifa.

"Vijana  wengi wa sasa hawakuishi na Mwalimu Nyerere  badala yake wamekuwa  wakizisikia falsafa za Mwalimu Nyerere kupitia utandawazi na vitabu mbalimbali pekee hivyo makongamano ya aina hii  yatasaidia kutoa elimu  kwa vijana,”alisisitiza Mhongole.


Hata hivyo  Mhadhiri wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Idara ya Jinsia Dkt. Tatu Nyange amesema  utafiti  alioufanya ambao ameuwasilisha katika kongamano hilo unahusu Uwazi na Uadilifu ni Masuala muhimu katika kuwajengea  uwezo vijana na  kizazi  cha sasa ili kiweze kuendelea na kufikia Maendeleo Endelevu.



Powered by Blogger.