WATANZANIA WATAKIWA KULINDA AMANI

 


Na Mwandishi wetu,DAR ES SALAAM 

KANISA  la Uamsho na Matengenezo ya Kiroho,limesema  kila Mtanzania  anajukumu la kuhakikisha anailinda  amani ya nchi na kuhakikisha inatawala na kutokuruhu watu wenye nia ovu kuivuruga

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam mapema leo Octoba 11,2024 na  Kiongozi wa kanisa hilo, Mwalimu Augustine  Tengwa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maono yake juu ya Taifa la Tanzania.

Amesema katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mtaa na Uchaguzi mkuu ni muhimu kila mmoja kuilinda amani ya Nchi pamoja kuwakemea ikiwemo kuwakataa watu au wanasiasa wachochezi.

"Natoa wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama katika kipindi  hiki cha kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mtaa na Uchaguzi mkuu kusimama vema katika nafasi zao ili kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaimarika kipindi hiki"amesema

Kiongozi huyo ambaye aliambatana na watumishi wezanke wa huduma hiyo yenye makao makuu yake Morogoro amesema  kupitia maombi ambayo wamekuwa wakiyafanya mfululizo, Mungu amewaonesha ishara ambayo si njema katika chaguzi zijazo nchini.

Hivyo amesema ni muhimu watanzania kwa pamoja kuungana na kumuomba Mungu ili aweze kuepusha ishara mbaya dhidi ya Taifa la Tanzania.

"Tanzania ni ya Watanzania na hawana taifa mbadala la kukimbilia iwapo wataruhusu wenye nia ovu kutimiza matakwa yao ili kupata nafasi za uongozi"amesema


Awali Mtumishi wa huduma hiyo Alpha Kiamba amewahimiza  Watanzania kuyapa kisogo maneno na taarifa zenye viashiria vya kuwagawa ambavyo vimekuwa vikizushwa na baadhi ya wanasiasa wakiwemo wanaharakati mbalimbali.

"Tunahitaji watu waombe, kila mkoa watu waingie kwenye maombi ya kukemea na kujaribu ishara zote mbaya dhidi ya Taifa la Tanzania..Sisi kama watumishi wa Mungu ni mabalozi wa Mungu."

Amesema, mara nyingi wamekuwa wakifanya maombi na wanaamini Tanzania bila maombi hakuna taifa.

Aidha amewaomba watanzania kutokuwa na kasumba ya kuupuza taarifa zinazotolewa watumishi wa Mungu kwani wao wametumwa na Mungu.

Powered by Blogger.