AQRB KUANZISHA VILABU VYA KUHAMASISHA MASOMO YA SAYANSI
Na Mwandishi Wetu,DAR ES SALAAM
BODI ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) inatarajia kuuanzisha Klabu za Kuhamasisha wanafunzi kupenda kusoma masomo ya Sayansi ili kuzalisha wataalamu wa kutosha kwenye fani hizo
Akizungumza kwenye zoezi la ugawaji wa zawadi kwa wanafunzi walioshiriki shindano la Insha kwa mwaka 2024/25 Ofisa Uhusiano wa bodi hiyo Hamisi Sungura amesema AQRB inalenga kuendelea kujikita kuwafahamisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari faida za kusoma fani za Ubunifu Majengo na Ukadiriaji Majenzi
Amesema awali walikuwa na utaratibu wa kuandaa mashindano ya uandishi wa Insha kuhusiana na fani hizo ili kuwajengea uelewa wanafunzi juu ya taaluma hizo jambo ambalo kwa kiasi kikibwa limeonesha uelewa kwa baadhi ya wanafunzi
" Kutokana na hali hiyo AQRB kwa sasa tumeazmia kusitisha mashindano ya uandishi wa insha na kuja na wazo jipya la kuanzisha vilabu vya kuhamasisha wanafunzi kuzifahamu fani hizo," ameisema Sungura
Ameongeza kuwa ili kuwa na wataalamu wa kutosha nchini Bodi ya AQRB ina wajibu wa kuendelea kuwahamasisha wanafunzi kuanzia ngazi ya msingi kuzifahamu fani hizo na kuzisomea ili kuliwezesha taifa kuwa na wataalamu wa kutosha
Kwa upande wake Mbunifu Majengo Halima Mrisho amesema ili mwanafunzi aweze kuwa Mbunifu Majengo au Mkadiriaji Majenzi ni lazima asome masomo ya sayansi
Amefafanua baadhi ya masomo ambayo hayakwepeki katika fani hizo kuwa ni pamoja na Hisabati, Fizikia Kemia ,baiolojia na Jiografia
Amewaasa wanafunzi nchini hususani wa kike kuacha kuyaogopa masomo haya kwa mtazamo wa kuwa ni magumu badala yake wayachukulie kuwa ni sawa na masomo mengine
Zaidi ya shule 300 za msingi na sekondari Tanzania Bara zimeshiriki mashindano ya insha yaliyoandaliwa na AQRB kwa mwaka 2024/25



