YANGA YAWAANGAMIZA MASHUJAA
Na Mwandishi wetu,DAR ES SALAAM
Timu ya Dar Salaam Young African imetoa kipigo cha mbwa mwizi kwa timu ya mashujaa football club.
Yanga ikiwa kwenye dimba lake la nyumbani la KMC complex imetoa kipigo hiko kikubwa zaidi kwenye ligi kuu ya NBC kwa msimu huu mpaka sasa cha goli 6 bila ya majibu.
Yanga ilionesha kandanda safi walianza kufungua kalamu hiyo ya magoli kupitia kwa mchezaji wao mpya aliyesajiliwa dirisha dogo aitwae Damaro mnamo dakika ya saba ya mchezo.
hadi kipenga cha mwisho kwenye uwanja wa KMC Complex Mashujaa amechezea kichapo kizito kutoka kwa Yamea Sc.
Yanga Sc 6 - 0 Mashujaa
Damaro ⚽
Abuya ⚽
Pacome ⚽
Dube ⚽
Mudathir ⚽
Depu ⚽

