SIMBA YAANZA KUNOGA MAREKEBISHO YA KATIBA

 


Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) imeidhinisha rasmi marekebisho ya Katiba ya klabu ya Simba baada ya kukamilika kwa mchakato wa kisheria uliokuwa chini ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Michezo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Februari 18, 2026, Msajili wa Vyama vya Michezo nchini, Abel Ngilangwa, amesema marekebisho hayo yamefanyika kwa kuzingatia Sheria na Kanuni zote zinazosimamia vyama vya michezo nchini.

Haya yanajiri siku mbili tu baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda mnamo Februari 16, 2026 kumuagiza Msajili wa Vyama vya Michezo kuhakikisha kuwa mchakato wa marekebisho ya Katiba ya Simba unapatiwa majibu kabla ya mwezi kumalizika.

"Napenda kuufahamisha umma kuwa mchakato wa uchambuzi, tathmini na uidhinishaji wa marekebisho ya Katiba ya Klabu ya Simba umekamilika kwa mujibu wa Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa Sura ya 49 na kanuni zake," - amesema Ngilungwa

Ngilangwa ameongeza kuwa Katiba hiyo iliyorekebishwa iliwasilishwa kwa mujibu wa Kanuni ya 11 ya Kanuni za Msajili wa Vyama vya Michezo T.S Na. 441 ya mwaka 1999 kwa ajili ya kupitiwa na kuidhinishwa.

Aidha ameeleza kuwa Msajili alitekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Kanuni ya 11(3)(a) ya Kanuni za Msajili wa Vyama vya Michezo T.S Na. 441 ya mwaka 1999, inayomtaka kuhakikisha marekebisho yoyote ya katiba hayaathiri usalama, hayavurugi amani miongoni mwa wanachama au jamii kwa ujumla, wala kuathiri maendeleo ya chama.



Powered by Blogger.