KAULI YA BAO HALALI LA SIMBA LILILOKATALIWA LAWAIBUA YANGA
Kauli ya Bao halali halafu limekataliwa ambayo imetolewa katika taarifa ya Bodi ya Ligi jana imezua maswali na kuwaacha watu midomo wazi.
Taarifa ya Bodi ya Ligi jana iliyotolewa ja Afisa habari wake Karim Boimanda na kusema Mwamuzi aliyekataa bao halali la Simba katika mchezo wa Watani wa jadi Simba na Yanga wa Ligi Kuu uliochezwa wikiendi iliyopita Visiwani Zanzibar, imeshindwa kueleweka vyema maana bao halali ni lile linalokubaliwa uwanjani na Mwamuzi wakati bao la Simba lilikataliwa sasa neno ‘halali’ limeleta maswali mengi.
Wengi wanahoji halali vipi na lilikataliwa uwanjani? Sasa kama halali mbona hawajapewa sasa?
Taarifa ya Bodi ya Ligi jana imezua maswali mengi kuhusu maamuzi yake katika mchezo huo wa Watani wa Jadi.
Kama halali sasa mbona hawajapewa Simba? Halali vipi na uwanjani lilikataliwa? Hayo ndio maswali yanayoendelea mitandaoni.

