MVUA YATIA DOA MECHI YA TRA NA SIMBA
Mchezo Kati ya wenyeji, TRA United dhidi ya Wekundu wa Msimbazi, Simba SC umeahirishwa rasmi kutokana na uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid, Kaloleni Jijini Arusha kujaa maji kutokakana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.
Kamishna wa mchezo huo wa Ligi kuu ya Soka ya NBC Tanzania bara, Musa Nyamandege ametangaza kuuahirisha mchezo huo kwa sababu ya mvua kubwa inayoendelea kunyesha Jijini humo na kubainisha kwamba Bodi ya Ligi ndiyo yenye jukumu la kupanga tarehe mpya ya mchezo huo na sio wao.


