MWAMUZI MECCHI YA SIMBA NA YANGA KIFUNGONI BAADA YAKUSHINDWA KUTAFSIRI SHERIA MECHI YA DERBY.
Hizi adhabu zilizotoka katika mchezo wa Derby ya Kariakoo ambao ulikuwa mchezo namba 54 wa Ligi Kuu uliopigwa Machi Mosi mwaka huu katika dimba la New Amaan Complex huko visiwani Zanzibar.
Mwamuzi msadizi namba moja Kassim Mpanga, kutoka jijini Dar es salaam, amefungiwa miezi sita kwa kuinyima Simba bao halali lililofungwa dakika ya 70 na Selemani Mwalimu.
Mwamuzi namba mbili Hamdan Said kutoka mkoani Mtwara, amefungiwa miezi mitatu kwa kuwanyima Yanga nafasi ya kufunga bao kupitia kwa Prince Dube dakika ya 61 akitafsiri ni offside.
Klabu ya Simba italazimika kulipa gharama za matengenezo ya mlango wa kuingilia katika chumba cha mikutano ya wanahabari kwakua walivunja wakati wakilazimisha kuingia kiwanjani.
Klabu ya Simba imetozwa faini ya Milioni 5 kwa kosa la kupita kwenye lango lisilo rasmi na Milioni 5 nyingine kwa kosa la kukataa kutumia chumba rasmi cha kuvalia.
Klabu ya Simba na Yanga zimetozwa faini ya shilingi Milioni 5 kila mmoja kwa kosa la walinzi wake kugombana na kutoleana lugha za matusi.
✍

