RAIS DKT.MWINYI AFUTURISHA WANANCHI WA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika futari ya pamoja aliyowaandalia wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.


Hafla hiyo imefanyika leo, tarehe 09 Machi 2026, katika Ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali, Mkokotoni, na imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, viongozi wa dini pamoja na waumini wa Dini ya Kiislamu. Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Mke wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Mama Mariam Mwinyi.


Alhaj Dkt. Mwinyi anaendeleza utaratibu wa kuandaa futari kwa wananchi unaofanyika katika mikoa yote mitano ya Zanzibar wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, na tayari amefanya hivyo katika mikoa miwili ikiwemo Mkoa wa Mjini Magharibi.




Powered by Blogger.