SENEGAL YAFANYA GWARIDE LA UBINGWA WA AFCON NCHINI UFARANSA

Senegal imelitambulisha Kombe la AFCON kwa Mashabiki zaidi ya 80,000 nchini Ufaransa kabla ya kuwavaa Peru kwenye mechi ya Kimataifa Kirafiki.


Senegal walitwaa kombe la Afrika baada ya kuichapa Morocco bao 1-0 katika fainali ambayo ilizua utata.


Hivi karibuni Shirikisho la soka barani Afrika CAF lilibatilisha ushindi wa Senegal na kuitangaza Morocco kuwa Mabingwa wa AFCON 2025 kwa madai ya timu ya taifa ya Senegal kukiuka baadhi ya kanuni.


Hata hivyo Senegal ilipinga hatua hiyo na kuamua kukata rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo CAS.

Powered by Blogger.