RAIS DKT MWINYI WATANZANIA WATAENDELEA KUMUENZI LUKUVI KWA MCHANGO WAKE WA UTUMISHI NCHINI



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Watanzania wataendelea kumkumbuka  na kumuenzi  Marehemu William Lukuvi kwa mchango wake wa utumishi  aliyotoa katika nyadhifa za uongozi mbalimbali alizoshika wakati wa uhai wake nchini ikiwemo kutatua changamoto za migogoro ya ardhi.


Dkt.Mwinyi ameyasema hayo katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Marehemu William Vangimembe Lukuvi, iliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam, leo tarehe 28 Machi 2026.


Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaongoza waombolezaji, wakiwemo viongozi mbalimbali wa kitaifa na wananchi, katika ibada hiyo ya kumuaga Marehemu Lukuvi.


Vilevile, viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa, dini na vyombo vya ulinzi na usalama wameshiriki katika ibada hiyo.


Marehemu William Lukuvi amefariki dunia tarehe 25 Machi 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma. Anatarajiwa kuzikwa tarehe 31 Machi 2026, kijijini kwao Idodi, Iringa Vijijini, mkoani Iringa.

Powered by Blogger.