KAMATI YA MAANDALIZI YA MAONESHO SABASABA 2026 YAKUTANA
Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Sabasaba 2026 imekutana katika makao makuu ya TanTrade kujadili mikakati ya kuboresha mchakato wa maandalizi ya maadhimisho ya miaka 50 ya SABASABA 2026.
Katika kikao hicho, Mkurugenzi wa TanTrade, Dkt. Latifa Khamis, aliwasilisha mkakati wa awali wa maandalizi, ukilenga kuhakikisha maonesho ya mwaka 2026 yanatekelezwa kwa viwango vya juu vya ubora na kuvutia washiriki wengi zaidi kutoka ndani na nje ya nchi.
Baada ya mawasilisho hayo, Mwenyekiti wa kikao, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Aristides Mbwasi, aliridhishwa na hatua zilizofikiwa katika maandalizi ya maonesho. Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuongeza kasi ya utekelezaji kwa kuwa maonesho haya ni ya kihistoria na yana nafasi kubwa katika kuchochea maendeleo ya biashara na uchumi wa taifa.



