MWENGE WA UHURU WAWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA UMEME MATEMWE AMBAO NI NEEMA YA UPATIKANAJI WA UMEME ZANZIBAR.

 


Mradi huo unaojengwa Matemwe mkoa wa Kaskazini A Unguja ,mkimbiza Mwenge  kitaifa ndugu Wazo Michael Mwang'onda alianza kwa kumpongeza Rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar DKT.Husein Mwinyi kwa nia yake ya dhati yakumaliza tatizo la upatikanaji wa umeme wa uhakika visiwani Zanzibar.



Pia ndugu Wazo Michael Mwang'onda alitumia wasaa huo kumpongeza meneja mkuu wa shirika la umeme Zanzibar ZECO mhandisi Haji Haji  kwa kusimamia ujenzi wa vituo hivyo vya kupozea umeme kwa namna yakizalendo na kwani maendeleo yake yanaonekana vilevile usimamizi wa wazi kabisa tangu utoaji wa zabuni ya ujenzi na pia upashaji taarifa kwa jamii inayozunguka miradi hiyo.




Awali meneja mkuu wa ZECO mhandisi Haji Haji akitolea maelezo yakitaalamu ya ujenzi wa mradi huo alitanabaisha kwamba mradi huu wa msongo wa KV 132 ni wa vituo vitatu ambapo kuna welezo,Makunduchi na huu wa Matemwe ambapo itapokea umeme moja kwa moja wa 132KV kutoka Dar es aalaam na kupoozwa kwenda 33KV na kusambazwa kwenda maeneo mbalimbali ya kaskizini unguja na viunga vyake ambapo mradi huo unatarajiwa kukamilika Novemba mwaka huu.

Powered by Blogger.