SERIKALI YAUNGANISHA MIFUMO 252 KWENYE MTANDAO

 


Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete amesema kuwa juhudi za Serikali katika kuwekeza katika TEHAMA zimeleta mageuzi makubwa katika utoaji wa huduma kwa wananchi, ikiwemo kurahisisha upatikanaji wake bila kulazimika kufika ofisini. 


Amezungumza hayo leo Aprili 17, 2026 Bungeni Dodoma,  wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora akieleza kuwa kati ya Julai 2025 na Machi 2026, jumla ya mifumo 252 ya Serikali imeunganishwa katika mtandao, hatua iliyopunguza muda na gharama kwa wananchi.


Akiongeza kuwa maboresho hayo yamechangia kupunguza urasimu uliokuwa ukikwamisha utoaji wa huduma, huku yakiongeza uwazi na kuimarisha uwajibikaji katika taasisi za umma.

#mwangwinews



Powered by Blogger.