TTCL YAPATA FAIDA NONO,YAZINDUA KITUO CHA KIDIGITALI KIJITONYAMA

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limetangaza kupata faida ya shilingi bilioni 22.9 kabla ya kodi kwa mwaka wa fedha 2024/25, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wake wa kujiendesha kibiashara.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, David Nchimbi, amesema mafanikio hayo yanachochea dhamira ya shirika kuongeza mapato na kudumisha faida endelevu kupitia ubunifu na usimamizi bora wa rasilimali.
Katika hatua nyingine, TTCL imezindua Kituo cha Kisasa cha FTTX Experience Center Kijitonyama, kitakachotoa elimu na uzoefu wa matumizi ya teknolojia za kidijitali kwa wananchi.
Nchimbi amepongeza ushirikiano kati ya TTCL, Huawei na Hisense katika kufanikisha mradi huo, akisisitiza umuhimu wa ubunifu na teknolojia katika maendeleo ya huduma za mawasiliano nchini.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Moremi Marwa, amesema mradi wa Faiba (FTTX) unalenga kusambaza intaneti yenye kasi na uhakika katika makazi, ofisi na biashara, hatua itakayochochea mageuzi ya kidijitali na ukuaji wa uchumi.
Amesema kituo hicho pia kitawawezesha wananchi kujifunza matumizi ya teknolojia za kisasa kama “smart home” na mifumo ya ofisi za kidijitali.

.jpeg)
.jpeg)