TANESCO YAENDELEA KUIMARISHA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME TABORA–KATAVI LICHA YA MAZINGIRA MAGUMU*

 


📍 Tabora – Katavi


Licha ya mazingira magumu yanayokabiliwa na njia ya kusafirisha umeme inayopita katika misitu minene yenye wanyamapori, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linaendelea kujituma kufanya matengenezo na maboresho ya njia ya umeme msongo wa kilovolti 132 kutoka Mkoa wa Tabora hadi Katavi.


Akizungumza wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo, Mhandisi Pius Josephat amesema uongozi wa TANESCO uliunda timu ya wataalamu 42 kutoka mikoa mbalimbali nchini, waliounganishwa na dhamira moja ya kuboresha huduma ya umeme hata katika mazingira magumu.


Hatua hizi zinaendelea kuihakikishia Katavi umeme wa uhakika badala ya kutegemea umeme wa mafuta kuzalisha umeme.





Powered by Blogger.