TASNIA YA BURUDANI YAPATA PIGO JINGINE MSANII SPACK AFARIKI DUNIA LEO

 



Wakati wasanii wa bongo movie wakiendelea kuombeleza kifo cha msanii Hashim Kambi wasanii wa bongo fleva nayo imepata  pigo kwa a



liyekuwa msanii wa Bongo Fleva, Selemani Mvamba almaarufu 'Spack', amefariki dunia leo Aprili 27, 2026 nyumbani kwake Chanika jijini Dar es Salaam alipokuwa anapoishi.


Meneja wa msanii huyo Abdulrahman Hassan almaarufu Malefti amethitibitisha kifo cha msanii huyo aliyejipatia umaarufu mkubwa kupitia kundi la Tip Top Connection, pamoja na nyimbo ya Nipe Ripoti aliyoshikiana na Tundaman.


Malefti amebainisha kwamba siku ya jana alizungumza na msanii huyo kuhusu mpango wao wa 'kushoot' video ya wimbo mpya kabla ya kuagana saa saba usiku na kubainisha kwamba asubuhi alienda kugongewa kwa ajili ya kutoa nauli za watoto kwenda shule akawa haamki.


Meneja huyo amesema baada ya yaliyotokea majirani walimpeleka hospitali ya Nguvu Kazi iliyopo Chanika ndipo daktari alithibitisha kuwa msanii huyo amefariki Dunia.



Powered by Blogger.