MWENYEKITI UVCCM TAIFA, KAWAIDA AFUNGUA MAFUNZO YA MAKATIBU WILAYA WA UVCCM

 


Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndugu Mohammed Ali Kawaida (MCC) amefungua mafunzo kwa Makatibu wa UVCCM wilaya zote Tanzania leo tarehe 14 Aprili 2026.


Mafunzo hayo yamehusisha pia Makatibu Wasaidizi wa UVCCM ngazi ya Mikoa ni sehemu ya mkakati wa Jumuiya ya UVCCM kuendelea kuimarisha uongozi na utendaji kazi wa viongozi wake katika ngazi mbalimbali. 


Makatibu hao kupitia mafunzo hayo, washiriki watapata fursa ya kujengewa uwezo katika maeneo muhimu ikiwemo uongozi bora, mawasiliano ya kisiasa, usimamizi wa shughuli za chama, pamoja na mbinu za kuhamasisha na kuunganisha vijana katika kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za maendeleo na za kisiasa.

Powered by Blogger.