WAZIRI NDEJEMBI AWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI 2026/27 BUNGENI

📌Asema kipaumbele ni kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini

📌 Uwezo wa uzalishaji umeme waongezeka kwa asilimia 12.17

📌Aeleza ongezeko hilo limechangiwa na kukamilika kwa miradi mbalimbali ya umeme

Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amewasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Bajeti  ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2026/2027, akiainisha vipaumbele  katika sekta ndogo ya umeme kuwa ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Akisoma hotuba ya bajeti hiyo Aprili 22, 2026, Bungeni Dodoma, Waziri Ndejembi ametaja vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na kuendeleza uzalishaji wa umeme kupitia mitambo tisa katika Kituo cha Kufua Umeme cha Bwawa la Julius Nyerere, kukamilisha awamu zinazofuata katika mradi wa kuzalisha umeme kwa nguvu ya jua Kishapu baada ya megawati 50 kuunganishwa kwenye gridi ya taifa na utekelezaji wa mradi wa umeme wa Malagarasi, Kigoma  unaotarajia kuzalisha Megawati 49.5 za umeme.

Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana katika eneo la uzalishaji  umeme, Waziri Ndejembi amesema hadi kufikia mwezi Machi 2026, uwezo wa kuzalisha umeme umeongezeka na kufikia jumla ya megawati 4,522.54 kutoka megawati 4,031.71 mwaka2025 ikiwa ni ongezeko la asilimia 12.17

Amesema ongezeko hili limetokana na kukamilika kwa miradi mbalimbali ya umeme, ukiwemo mradi wa kuzalisha umeme kwa nguvu ya jua Kishapu (awamu ya kwanza) unaozalisha jumla ya megawati 50.

Aidha, katika eneo la usafirishaji, amesema hadi kufikia mwezi Machi 2026, urefu wa miundombinu ya kusafirisha umeme nchini ulikuwa umefikia jumla ya kilomita 8,500.38 kutoka kilomita 7,809.67 mwezi Machi 2025.

“Hadi kufikia Machi 2026, urefu wa miundombinu ya kusafirisha umeme nchini ulikuwa umefikia kilomita 8,500.38 ikilinganishwa na kilomita 7,809.67 zilizokuwepo Machi 2025, sawa na ongezeko la asilimia 9,” alisema.

Amesisitiza kuwa Serikali, kupitia TANESCO, imeendelea kuimarisha huduma kwa wateja kwa kuboresha mifumo ya kidijitali, ambapo ilizindua mita janja (smart meters) zinazowezesha umeme ulionunuliwa na mteja kuingia moja kwa moja kwenye mita.

“Hadi kufikia Machi 2026, jumla ya wateja 105,739 walikuwa wameunganishwa na mita janja, na zoezi hilo linaendelea kwa awamu katika maeneo yote ya nchi,” alieleza Mhe. Ndejembi.

Waziri Ndejembi pia amefafanua kuwa kutokana na hatua zilizochukuliwa katika ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme, kiwango cha upatikanaji wa umeme nchini kimeongezeka kutoka wastani wa asilimia 78.4 mwaka 2020 hadi kufikia wastani wa asilimia 85.5.WAZIRI NDEJEMBI AWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI 2026/27 BUNGENI

📌Asema kipaumbele ni kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini

📌 Uwezo wa uzalishaji umeme waongezeka kwa asilimia 12.17

📌Aeleza ongezeko hilo limechangiwa na kukamilika kwa miradi mbalimbali ya umeme

Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amewasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2026/2027, akiainisha vipaumbele katika sekta ndogo ya umeme kuwa ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Akisoma hotuba ya bajeti hiyo Aprili 22, 2026, Bungeni Dodoma, Waziri Ndejembi ametaja vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na kuendeleza uzalishaji wa umeme kupitia mitambo tisa katika Kituo cha Kufua Umeme cha Bwawa la Julius Nyerere, kukamilisha awamu zinazofuata katika mradi wa kuzalisha umeme kwa nguvu ya jua Kishapu baada ya megawati 50 kuunganishwa kwenye gridi ya taifa na utekelezaji wa mradi wa umeme wa Malagarasi, Kigoma unaotarajia kuzalisha Megawati 49.5 za umeme.

Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana katika eneo la uzalishaji umeme, Waziri Ndejembi amesema hadi kufikia mwezi Machi 2026, uwezo wa kuzalisha umeme umeongezeka na kufikia jumla ya megawati 4,522.54 kutoka megawati 4,031.71 mwaka2025 ikiwa ni ongezeko la asilimia 12.17

Amesema ongezeko hili limetokana na kukamilika kwa miradi mbalimbali ya umeme, ukiwemo mradi wa kuzalisha umeme kwa nguvu ya jua Kishapu (awamu ya kwanza) unaozalisha jumla ya megawati 50.

Aidha, katika eneo la usafirishaji, amesema hadi kufikia mwezi Machi 2026, urefu wa miundombinu ya kusafirisha umeme nchini ulikuwa umefikia jumla ya kilomita 8,500.38 kutoka kilomita 7,809.67 mwezi Machi 2025.

“Hadi kufikia Machi 2026, urefu wa miundombinu ya kusafirisha umeme nchini ulikuwa umefikia kilomita 8,500.38 ikilinganishwa na kilomita 7,809.67 zilizokuwepo Machi 2025, sawa na ongezeko la asilimia 9,” alisema.

Amesisitiza kuwa Serikali, kupitia TANESCO, imeendelea kuimarisha huduma kwa wateja kwa kuboresha mifumo ya kidijitali, ambapo ilizindua mita janja (smart meters) zinazowezesha umeme ulionunuliwa na mteja kuingia moja kwa moja kwenye mita.

“Hadi kufikia Machi 2026, jumla ya wateja 105,739 walikuwa wameunganishwa na mita janja, na zoezi hilo linaendelea kwa awamu katika maeneo yote ya nchi,” alieleza Mhe. Ndejembi.

Waziri Ndejembi pia amefafanua kuwa kutokana na hatua zilizochukuliwa katika ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme, kiwango cha upatikanaji wa umeme nchini kimeongezeka kutoka wastani wa asilimia 78.4 mwaka 2020 hadi kufikia wastani wa asilimia 85.5.

Powered by Blogger.